PRECISION AIR YAANZISHA MPANGO WA MAFUNZO KAZINI KUTATUA UHABA WA WAHANDISI SEKTA YA ANGA TANZANIA

19 Julai 2018….Shirika la Ndege la Precision Air limezindua mpango maalumu wa mafunzo kazini kwa ajili ya vijana wa Kitanzania wenye ndoto za kua wahandisi wa Ndege siku za usoni. Precision Air imezindua programu hiyo makhususi kukabiliana na uhaba wa wahandisi katika sekta ya anga nchini.

Shirika la Ndege la Precision Air, ambalo ndilo shirika pekee nchini lenye leseni ya kufanya matengenezo ya ndege, limeanzisha mpango huo kwa katika jitihada za kuendeleza rasilimali watu inayohitajika katika katika kitengo chake cha ufundi kupitia mafunzo maalumu kwa wanafunzi wa ufundi pamoja na mpango wa mafunzo kazini.
Katika kumpuo wa kwanza Precision Air limeajiri mafundi 22 kupitia mpango wa mafunzo kazini katika kitengo chake cha Uhandisi na ufundi. Mafundi hao watakua wkifanya akazi huku wakiendelea na mafunzo ya vitendo.
Akizungumzia mpango huo, Mkurugenzi Mkuu wa Precision Air, Bi.Sauda Rajab amesema, upatikanaji wa rasilimali watu katika sekta ya anga umekua changamoto kubwa nchini. Ameongeza kuwa Precision Air kama shirika lenye uzoefu haliwezi kubaki kulalamika na ndo sababu shirika limechukua hatua ya kuanzisha mpango huo ili kusaidia katika kutatua tatizo.
“Tunajivunia mchango wetu katika kuendeleza rasilimali watu wenye ujuzi unaohitajika katika sekta ya anga Tanzania.Kupitia mpango wetu huu wa mafunzo kazini nimatumaini yetu tutaweza kutengeneza wahandisi wengi wa ndege ili kuweza kukidhi mahitaji ya soko na mahitaji yetu kama shirika.

Kwa upande mwingine Bi.Rajab, ameleza kuwa inachukua takribani miaka nane (8) kumuandaa Muhandisi kamili mwenye leseni, huku pia ikigharimu fedha nyingi katika kusomesha wahandisi, hivyo anatarajia wadau wengine kwenye sekta ya anga watafanya jitihada kama za Precision Air, badala ya kutegemea wataalamu kutoka njee pekee, ili kuimarisha sekta na kutengeneza ajira nyingi zaidi kwa vijana wa Kitanzania.

Shirika la ndege la Precision Air pia lilisaini mkataba na Chuo cha Usafirashaji (NIT) mnamo mwaka 2017, mkataba unaowawezeshan wanafunzi kutoka chuo hiko kupata nafasi za mafunzo ya vitendo katika shirika la Precision Air na kwa kuzingatia uwezo wa wanafunzi wanfunzi hao wana nafasi ya kupata ajira ya moja kwa moja katika shirika hilo. Hadi sasa Kupitia mkataba huo Precision Air imeshatoa mafunzo kwa wanafunzi 33.
Shirika la Ndege la Precision Air lilianzishwa mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi, likifanya safari zake kusafirisha watalii katika vivutio vya utalii kama Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro pamoja na Visiwa vya Zanzibar. Sasa Shirika hilo lenye makoa yake makuu katika Jiji la Dar es Salaam limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika yanayo heshimika katika ukanda wa Africa Mashariki na Africa kwa ujumla.Ikifanya safari zake kutokea Dar es Salaam, Precision Air inasafiri kuelekea Arusha, Bukoba, Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza, Tabora, Kahama, Zanzibar,Nairobi na Entebbe.